Yanga yafanya tathmini ya hasara

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Mar 2025
Yanga yafanya tathmini ya hasara

Yanga ilikuwa mwenyeji wa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao ulipaswa kupigwa Jumamosi March 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga imebainisha kuwa mabingwa hao wa Tanzania Bara wanafanya tathmini ya hasara waliyopata na watadai fidia kwa kitendo cha Bodi ya ligi kuahirisha mchezo huo zikiwa zimebaki saa chache kabla ya kuchezwa

Juzi baada ya mchezo kuahirishwa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alisema hadi kufikia saa 7 mchana siku ya mchezo, mashabiki 40,000 walikata tiketi

Kamwe alisema mamlaka zitafanya tathmini na akawahakikishia mashabiki waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo kuwa haki zao zitalindwa

"Viongozi wanafanya tathmini ya hasara iliyosababishwa na kuahirishwa kwa mchezo dhidi ya Simba siku ya Jumamosi"

"Kuna gharama kubwa zilizopatikana kuanzia maandalizi ya kambi, matangazo na mambo mengine, hivyo sio rahisi kufahamika mara moja, ndio maana wanakutana kwa sasa kuweka sawa, ila ukweli ni kwamba Yanga imepata hasara za mamilioni ya fedha kwa sababu ya ubinafsi wa wachache," alisema mtoa taarifa

Yanga imejipanga kudai haki yake katika mamlaka za juu kama itatokea hawatapewa haki hiyo na mamlaka za ndani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’