Jana kikosi cha Yanga kilitinga hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la Shirikisho la CRDB (FA) baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex
Ushindi huo ulikuwa wa 20 mfululizo kwa Yanga katika michuano hiyo n hivyo kuweka rekodi ya kibabe
Yanga imetwaa mataji matatu mfululizo ya michuano hiyo, ikishinda mechi 18
Katika msimu huu Wananchi wameshinda mechi 2 na hivyo kufikisha idadi ya mechi 20
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema malengo ni kutwaa taji hilo kwa msimu wa nne mfululizo
Mchezo unaofuata kuwania tiketi ya kutinga robo fainali Wananchi watacheza dhidi ya Songea United
ADVERTISE HERE