Yanga yatoa mapumziko kwa wachezaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Mar 2025
Yanga yatoa mapumziko kwa wachezaji

Baada ya kukamilisha mchezo wa hatua ya 32 bora kombe la Shirikisho la CRDB kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Coastal Union jana, Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi ametoa mapumziko ya siku 6 kwa wachezaji

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema wakati huu ambao ligi inasimama kupisha kalenda ya FIFA, wachezaji ambao hawatakuwa katika majukumu ya timu za Taifa watanufaika na mapumziko hayo na watakaporejea watakuwa na kazi ya kuhitimisha mechi zilizosalia ligi kuu na kombe la CRDB

"Klabu imetoa mapumziko ya siku sita kwa wachezaji wetu. Lengo ni kuwapa nafasi ya kujiandaa"

"Tumebakiwa na michezo migumu sana. Kila mechi ngumu kwa sababu watu ndio wanaelekea kufunga biashara. Kuna wanaoshuka, kuna wanaotaka nafasi za juu. Kila mtu anapambania malengo yake," alisema Kamwe

Katika hatua nyingine, Kamwe amesema klabu ya Yanga imeandaa tukio maalum la Iftar ambapo imewaalika wadau mbalimbali wa soka nchini kujumuika pamoja

"Yanga tumeandaa Iftari kwa wadau wetu na washirika wetu mbalimbali. Tumewaalika TFF, Bodi ya ligi (TPLB), waamuzi pamoja na vilabu vingine vya ligi kuu. Nimemualika Ahmed Ally na amenijibu atakuja na watu wawili ambao ni Steven Mguto na Almasi Kasongo," alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’