Siku tatu ambazo klabu ya Yanga ilizitoa kwa Bodi ya ligi wakiomba kupatiwa alama tatu baada ya kutofanyika kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba, zimemalizika
Yanga sasa inajipanga kufungua shauri katika Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa michezo (CAS) kuziomba alama hizo tatu baada ya klabu ya Simba kukacha mchezo wa dabi Jumamosi iliyopita huku 'wakikingiwa kifua' na Bodi ya Ligi
Yanga inapinga hatua ya Bodi ya Ligi kuuahirisha mchezo huo uliotakiwa kuchezwa Machi 8 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam bila kuzingatia kanuni zinazosimamia Ligi.
Taarifa za ndani ya uongozi, zimedokeza kuwa takribani wanasheria 9 wataiwakilisha Yanga katika shauri hilo
Kumekuwa na jitihada za kuirudisha Yanga mezani kwa mazungumzo, lakini viongozi wa Yanga wameshikilia msimamo kutoshiriki hasa ikizingatiwa, msimamo wa kutocheza mechi dhidi ya Simba unaungwa mkono kwa asilimia 100 na mashabiki na wanachama wa Yanga