Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema msafara wa timu hiyo utaondoka jijini Dar es salaam Jumamosi March 22 kuelekea mkoani Singida kushiriki uzinduzi wa uwanja wa Singida Black Stars (Airtel Stadium)
Jumatatu, March 24 tukio la uzinduzi huo litafanyika ambapo mechi ya kirafiki kati ya Singida Black Stars dhidi ya Yanga itachezwa katika uwanja huo
Kamwe amesema timu ilirejea mazoezini jana na wanakwenda Singida wakiwa na wachezaji wote ambao hawakuitwa katika majukumu ya timu za Taifa
"Kikosi kimerejea mazoezini na siku ya Jumamosi tunatarajiwa kuondoka Dar es salaam kuelekea Singida ambako tumealikwa na Singida Black Stars kushiriki tukio la uzinduzi wa uwanja wao"
"Tutaondoka na usafiri wa treni ya SGR hadi mkoani Dodoma ambako tutaunganisha kuelekea Singida kupitia usafiri wa basi"
"Wachezaji wote ambao hawakuitwa katika majukumu ya timu za Taifa watakuwepo akina Maxi Nzengeli, Pacome na Aziz Ki ni sehemu ya wachezaji watakaokuwepo"
"Tunawaambia Singida wamefanya kosa kubwa kutualika katika tukio hili la kihistoria kwani tutawafunga hapohapo kwenye uwanja wao katika siku hiyo muhimu ya uzinduzi," alisema Kamwe