Mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra ameendelea kuaminiwa katika timu ya Taifa ya Mali usiku wa kuamkia leo akikaa langoni Mali ikipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Comoros katika mchezo wa kuwania kufuzu kombe la Dunia 2026
Diarra anaendelea kuipeperusha vyema bendera ya Yanga Kimataifa, akiwa mchezaji pekee anayecheza ndani ya Afrika katika kikosi kilichoanza
Aidha nyota wengine wa Yanga jana walikuwa viwanjani kuzitumikia timu zao za Taifa
Khalid Aucho aliiongoza Uganda katika mchezo dhidi ya Msumbiji uliomalizika kwa Uganda kufungwa mabao 3-1
Mwana wa Mfalme Prince Dube akaanza katika kikosi cha Zimbabwe kilicholazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Benin
Duke Abuya nae alikuwa sehemu ya kikosi cha Kenya kilichopata sare ya mabao 3-3 ugenini dhidi ya Gambia