Wachezaji Kennedy Musonda na Clatous Chama kutoka klabu ya Yanga ni miongoni mwa wachezaji 19 waliojumuishwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Zambia kitakachocheza mechi ya Kimataifa ya kirafiki dhidi ya Urusi March 25
Zambia ambayo iko kundi E na Tanzania katika kinyang'anyiro cha kuwania kufuzu kombe la Dunia 2026, haitakuwa na mechi wakati huu baada ya Congo kufungiwa na FIFA
Ikumbukwe Eritrea ambayo ilikuwa kundi E pia ilijitoa na hivyo mechi zinazohusisha timu hizo hazitachezwa
Kocha wa Zambia Avram Grant ameteua kikosi cha wachezaji 19 kwa ajili ya mchezo huo akiwajumuisha Musonda na Chama ambao ni kama wamejihakikishia namba katika kikosi chake

Musonda alikuwa mfungaji kinara wa Zambia katika mechi za kuwania kufuzu Afcon 2025 akipachika mabao 4 na kuisaidia Zambia kukata tiketi ya michuano hiyo
Licha ya kutoanza katika kikosi cha Yanga, Musonda ndiye mshambuliaji tegemeo wa timu ya Taifa ya Zambia