Stars yatua Morocco

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Mar 2025
Stars yatua Morocco

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kimewasili nchini Morocco tayari kwa mchezo wa kuwania kufuzu kombe la Dunia 2026 kundi E dhidi ya wenyeji wao, Morocco

Mchezo huo utapigwa March 26 kwenye uwanja wa Honneur uliopo Manispaa ya d'Oujda, saa 6:30 usiku hapo Morocco

Ikiwa inashika nafasi ya tatu kundi E ikiwa na alama 6, Stars haipaswi kupoteza mchezo huo ili kusalia katika kinyang'anyiro cha kuwania tiketi ya kufuzu kombe la Dunia

Jana Morocco ilizidi kujichimbia kileleni baada ya kuichapa Niger bao 1-0 na hivyo kufikisha alama 12 wakiwa wameshinda mechi zote nne

Mechi pekee ambayo Tanzania imepoteza katika michuano hiyo, ilifungwa na Morocco mabao 2-0 katika mechi ya kwanza iliyopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Hivyo hii ni mechi ya kisasi kwa Stars dhidi ya timu hiyo namba moja kwa ubora Afrika kwa mujibu wa viwango vya FIFA

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’