Afisa Habari wa Singida Black Stars Hussein Massanza amesema wamempa baraka zote kocha Miloud Hamdi kuitumikia Yanga baada ya kumaliza mgogoro baina yake na klabu hiyo
Wakati Yanga inamtambulisha Hamdi kuchukua nafasi ya Sead Ramovic aliyetimkia CR Belouizdad, Singida BS walidai kocha huyo bado ana mkataba na walima alizeti hao na hivyo hawaungi mkono utaratibu wake wa kuondoka
Massanza amesema pande zote zimekutana na kumaliza sintofahamu hiyo hivyo kwa sasa hawana kinyongo na Hamdi wakimtakia kila la kheri katika majukumu yake kunako klabu ya Yanga
"Siku kocha Hamdi alipotambulishwa na Yanga tulisema tumestushwa na hatua hiyo kwa sababu kuna mambo hayakuwa yamefanyika kwa kufuata utaratibu"
"Lakini sasa jambo hilo limemalizika, mambo yakimkataba yamemalizwa baada ya pande zote kukutana mezani na wenzetu kulipa gharama ambazo walipaswa kuzilipa"
"Kwa sasa hatuna kesi tena na kocha Miloud Hamdi baada ya kutulipa, tunamtakia kila la kheri katika majukumu yake huko Yanga," alisema Massanza
Singida Black Stars ilimleta Miloud kuchukua mikoba ya Patrick Aussems aliyekuwa amefutwa kazi na timu hiyo
Hata hiyo aliingoza timu hiyo kwa siku 36 tu na akaibuka klabu ya Yanga ambayo iliachana na Ramovic aliyekimbilia CR Belouizdad alikopata ofa nono