Kesho Jumamosi March 29 katika uwanja wa KMC Complex, Yanga itaikaribisha Songea United katika mchezo wa hatua ya 16 bora kombe la Shirikisho la CRDB Wananchi wakisaka nafasi ya kutinga robo fainali
Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi ameendelea kukiandaa kikosi chake kwa ajili ya mchezo huo ambapo leo Wananchi watakamilisha maandalizi yao
Yanga itatumia mchezo dhidi ya Songea United kama sehemu ya maandalizi yake kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tabora United utakaopigwa April 2 katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora
Wakiwa mabingwa wa taji la FA kwa misimu mitatu mfululizo, malengo ni kutwaa taji hilo kwa msimu wa nne



ADVERTISE HERE