Ushindi dhidi ya Coastal Union ni muhimu - Hamdi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Apr 2025
Ushindi dhidi ya Coastal Union ni muhimu - Hamdi

Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema ilikuwa muhimu kwa kikosi chake kupata ushindi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union, amefurahi kwa kuwa wamelifanikisha

Hata hivyo Hamdi amesema walistahili kupata ushindi mnono zaidi katika mchezo huo walioshinda bao 1-0 lakini pengine walikosa umakini katika eneo la mwisho

Hamdi ambaye tangu alipotua Yanga hajapoteza mchezo wowote, amesema Alhamisi wanakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Azam Fc, hivyo ushindi huo unawafanya waende kwenye mchezo huo wakiwa na fikra chanya zaidi

"Ilikuwa muhimu kwetu kupata ushindi leo hivyo nafurahi tumefanikiwa ingawa tungeweza kufanya vizuri zaidi"

"Tulipata nafasi sita za kufunga mabao, nafahamu mashabiki wetu wanafurahi tukifunga mabao mengi lakini kwa leo niseme tunapaswa kufurahi kwa kuwa tumeshinda"

"Tumecheza mechi hii tukitoka kwenye mechi ngumu dhidi ya Tabora United na ndani ya muda wa siku mbili tunakabiliwa na mechi nyingine ngumu dhidi ya Azam Fc"

"Tuko juu katika msimamo wa ligi hivyo tunapaswa kuendelea kufanya vizuri katika kila mechi ili tuweze kufikia malengo yetu," alisema Hamdi

Yanga ina siku mbili za kukamilisha maandalizi yake kabla ya kuikabili Azam Fc katika mchezo utakaopigwa Alhamisi, April 10 katika uwanja wa Azam Complex

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’