Mshambuliaji kinara wa Yanga Prince Dube leo ameondoka na tuzo nyingine ya nyota wa mchezo akiisaidia Yanga kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex
Unaweza kusema Dube leo amewaadhibu waajiri wake wa zamani sawasawa akifunga na kutoa asisti katika uwanja aliozoea kufunga
Dube amerudi juu katika mbio za ufungaji bora akifikisha mabao 12 huku pia akiwa na asisti 8
Ukizingatia changamoto alizokutana nazo wakati anapambana kukamilisha uhamisho wake kujiunga na Yanga, kwa hakika leo ni siku ya furaha kwake..
ADVERTISE HERE