Prince Dube alibeba tuzo ya nyota wa mchezo wa ligi kuu kati ya Azam Fc dhidi ya Yanga uliopigwa Alhamisi usiku, April 10 katika uwanja wa Azam Complex
Katika mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, Dube alifunga bao la pili huku pia akitoa asisti ya bao la kwanza lililofungwa na Pacome Zouzoua
Unaweza kusema ni kwa sababu watoaji tuzo mara nyingi wanaangalia mabao na asisti lakini kama wangetumia vigezo vingine mfano kiwango cha jumla cha mchezaji, ni wazi tuzo huyo wangeweza kumpa Duke Abuya
Akishirikiana na vyema na Mudathir Yahya na Maxi Nzengeli, waliipoteza kabisa Azam Fc kwenye eneo la kiungo hasa katika dakika zote 45 za kipindi cha kwanza
Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi ameendelea kumuamini Abuya katika nyakati zote ambazo Khalid Aucho amekosekana kikosini
Abuya ni mchezaji kiraka ambaye amekuwa akitumika kwa kuzingatia mahitaji ya timu ingawa awali alisajiliwa kama kiungo mshambuliaji/winga
Hamdi ameonyesha kumuamini eneo la kiungo cha chini na sasa ni mchezaji mwenye uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza