Dube afurahia msimu bora bila majeruhi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Apr 2025
Dube afurahia msimu bora bila majeruhi

Tangu mshambuliaji Prince Dube aanze kucheza Ligi Kuu Bara 2020/21, amesema huu wa sasa ndio anaamini kwamba una tofauti katika maisha yake ya soka, huku akidai kuna kitu cha zaidi kinakuja.

Dube amefafanua kauli yake kwamba ilikuwa kawaida kuumia kila msimu tofauti na sasa ambapo anafurahia kucheza mechi nyingi bila majeraha.

Mshambuliaji huyo aliyetua Yanga msimu huu akitokea Azam katika ligi amehusika na mabao 20 kati ya 64 yaliyofungwa na timu hiyo kupitia nyota 13 tofauti.

Dube ambaye huu ni msimu wa tano katika Ligi Kuu Bara hadi sasa ndiye mchezaji kwenye ligi hiyo aliyehusika na mabao mengi msimu huu akifunga 12 na asisti nane.

"Nakiri kuwa huu ndio msimu wangu bora nimefunga mabao 12 nikiwatengenezea wenzangu mabao nane. Ukiondoa hilo nimeweza kuwa imara bila kuumia. Namshukuru sana Mungu na natamani kuona namaliza msimu bila ya kupata shida yoyote"

"Bado nina nafasi ya kufanya mambo mazuri na nitafanya hivyo kila nitakapopata nafasi. Namuomba Mungu nimalize msimu nikicheza mechi zote na kuipa timu yangu matokeo mazuri bila kujali nitafunga au nitatengeneza nafasi," alisema Dube

Akimzungumzia mchezaji huyo, kocha wa Yanga, Miloud Hamdi alisema anavutiwa na upambanaji wa Dube eneo la ushambuliaji akidai kuwa sio mchezaji mchoyo ndio maana amekuwa na mafanikio makubwa.

"Dube ni mpambanaji amekuwa bora licha ya kukosa nafasi nyingi sio mtu wa kukata tamaa. Anapambana kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri. Asipofunga, basi atatengeneza nafasi ya kufunga kama alivyofanya kwenye mchezo dhidi ya Azam FC"

"Mshambuliaji kazi yake ni kufunga na ni mchoyo, lakini hilo ni tofauti kwa Dube. Naamini anachofanya kitampa namba nyingi kwenye kufunga na hata kutengeneza nafasi, lakini nawapongeza wachezaji wote kuipambania timu," Hamdi alinukuliwa na Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’