Dozi ya Fountain Gate imeandaliwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Apr 2025
Dozi ya Fountain Gate imeandaliwa

Kikosi cha Yanga leo kimekamilisha maandalizi yake jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea Manyara kuikabili Fountain Gate katika mchezo wa ligi kuu ya NBC ambao utapigwa Jumatatu, April 21 katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa

Yanga inatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam kuelekea Manyara wakipitia mkoani Dodoma

Vinara hao wa ligi kuu wakiwa na alama 67 baada ya mechi 25, wamebakisha mechi nne tu za kuhakikisha ubingwa wa ligi unarejea kabatini pale Jangwani

Alama tatu za mchezo dhidi ya Fountain Gate zitaisogeza Yanga karibu kabisa ya kutimiza lengo lake la kutetea ubingwa

Wakati watani zao Simba wakiendelea 'kurundikiwa' viporo, Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi ameweka wazi kuwa hakuna nafasi ya kufanya makosa katika mechi zilizosalia

Kwa jinsi ratiba ilivyo kama Yanga itashinda mechi zote itatwaa ubingwa pasipo kujali matokeo ya watani zao

Ikumbukwe pia Yanga imeweka msimamo, inazipigania alama tatu za mchezo dhidi ya Simba uliopaswa kupigwa March 08 lakini haukufanyika

Yanga ina matumaini ya kushinda kesi yake iliyofungua CAS dhidi ya mamlaka za usimamizi wa soka nchini (TFF, TPLB) pamoja na klabu ya Simba 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’