Hamdi afunguka maandalizi mchezo dhidi ya Fountain Gate

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Apr 2025
Hamdi afunguka maandalizi mchezo dhidi ya Fountain Gate

Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi ameeleza kufurahishwa na wingi wa mashabiki wa timu hiyo waliojitokeza jana kuwapokea mabingwa hao wa nchi walipotua Babati tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Fountain Gate

Akizungumza katika Mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo utakaopigwa kesho Jumatatu katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Hamdi amesema mashabiki wa Yanga wameendelea kumshangaza kila anapokwenda akitaja sapoti yao inawaongezea wachezaji morali ya kupambana katika kila mechi

"Tumetayarisha mechi hii kwa namna ileile kama mechi nyingine zote kwetu sisi kila mechi ni muhimu sana"

"Lakini kabla sijazungumzia mechi ya kesho, ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa mashabiki waliokuja kwa wingi jana walikuwa wa kipekee"

"Sina maneno ya kuelezea vizuri, lakini wanapaswa kujua kuwa walitugusa sana mimi pamoja na wachezaji wote. Ilikuwa furaha kubwa kuwaona kwa wingi namna ile asanteni sana kwa sapoti yenu," alisema Hamdi

Aidha Hamdi ambaye ameiongoza Yanga katika mechi 11 akishinda 10 na kutoka sare mechi moja, amesema amekiandaa kikosi chake kimbinu kuikabili Fountain Gate

Amesema anaamini wachezaji wake watatafsiri vyema mpango wa mchezo huo na kuibuka na ushindi

"Lazima tuwe makini sana, tushinde kila mechi. Pia, tumefanya mikutano ya kiufundi, tumeangalia video na kufanya mazoezi ya kiufundi ili kujiandaa vizuri"

"Ninawaambia mara nyingi nyota wa mchezo ni mfumo. Wachezaji wote wakielewa mfumo, tutashinda mechi nyingi. Tuna wachezaji wenye uwezo wa kufanya mfumo ufanye kazi lakini jambo la kwanza ni kuelewa mfumo"

"Kwa hiyo mchezaji anapobadilishwa au kuingia uwanjani, lazima ajue moja kwa moja anachotakiwa kufanya na kile asichopaswa kufanya na kuelewa wa Wachezaji wangu naamini tutaendelea kufanya vizuri kwenye kila mchezo"

Hamdi amekiri baadhi ya wachezaji wake wana changamoto za majeruhi na maumivu ya hapa na pale lakini amesema yeye anaamini ana timu imara na ataendelea na utaratibu wa kumpa nafasi kila mchezaji

"Ni kweli tuna baadhi ya wachezaji majeruhi kama Aucho, Pacome bado hajawa tayari, Musonda anahisi maumivu kidogo si makubwa lakini hatuwezi kumuhatarisha pamoja na Azizi Ki ana maumivu ya muda mrefu"

"Nawaheshimu wachezaji wote. Mimi si kocha wa kulalamika kwamba sina huyu au yule hapana nitampa nafasi kila mchezaji. Hiyo ndiyo njia pekee ambayo itatuwezesha kufika mwezi Mei tukiwa imara, kwa sababu kila mchezaji atakuwa amepewa muda wa kucheza. Hilo ni jambo muhimu sana kwangu," aliongeza Hamdi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’