Yanga imetinga nusu fainali ya kombe la Muungano baada ya kuichapa KVZ mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Gombani, Pemba
Mabao ya Stephane Aziz Ki na Denis Nkane yametosha kuihakikishia Yanga ushindi katika mchezo huo ambao Wananchi walitawala kwa muda mwingi
Kama vijana wa kocha Miloud Hamdi wangekuwa makini, pengine wangeondoka na ushindi mnono zaidi
Yanga sasa itachuana Zimamoto katika mchezo wa nusu fainali utakaopigwa April 29
Mchezo wa kwanza wa nusu fainali utazikutanisha JKU dhidi ya Azam Fc
ADVERTISE HERE