Yanga imekuwa kivutio Pemba ikipata sapoti sapoti kubwa ya mashabiki tangu ilipotua siku ya Jumamosi kushiriki michuano ya ligi ya Muungano
Katika mchezo wa robo fainali ambao walicheza na KVZ, idadi kubwa ya mashabiki walijitokeza dimba la Gombani kuwashuhudia Wananchi
Leo Yanga inashuka tena Gombani kuikabili Zimamoto katika mchezo wa nusu fainali
Matarajio ni kuwa uwanja wa Gombani leo hautatosha! kwani mwamko wa mashabiki ni mkubwa
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema tiketi zimeanza kuuzwa mapema majira ya saa 2
"Kwa mara ya kwanza katika Historia ya Mpira hapa Pemba, Leo Tiketi zimeanza kununuliwa saa 2:00 asubuhi.. Kila mtu Hapa Pemba ana shauku ya kuiona Yanga leo ikicheza Nusu Fainali Hapa," alisema Kamwe
Mchezo unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 1:15 usiku Wananchi wakisaka tiketi ya kucheza fainali ya michuano hiyo