Hersi anahitaji pongezi kwa hili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Apr 2025
Hersi anahitaji pongezi kwa hili

Katika misimu ya nyuma, kanuni zilizotumika kupata timu zilizotinga hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho (CAF CC) zilikuwa tofauti ukilinganisha na kanuni zilizotumika msimu huu

Zamani ilikuwa timu zilizotolewa kwenye ligi ya mabingwa raundi ya mwisho kuelekea makundi zilipewa fursa ya kucheza raundi ya mwisho kombe la Shirikisho na zinaposhinda zinakwenda kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo

Msimu wa 2022/23 ambayo Yanga ilicheza fainali ya kombe la Shirikisho, ilinufaika na kanuni hiyo ambapo baada ya kutolewa na Al Hilal katika ligi ya mabingwa ilicheza raundi ya mwisho ya mtoano kombe la Shirikisho na kufanikiwa kutinga makundi baada ya ushindi dhidi ya Club Africain

Katika mwaka wake wa kwanza kwenye uongozi wake kama Mwenyekiti wa umoja wa vilabu barani Afrika (ACA), Injinia Hersi Said alipendekeza kanuni hiyo ibadilishwe ili timu zinazocheza ligi ya mabingwa zisipate fursa ya kwenda Shirikisho zinaposhindwa kutinga makundi CAF CL

Hii ni kwa sababu mara nyingi timu zinazocheza CAF CL ni mabingwa wa nchi zao au zile zinazomaliza katika nafasi ya pili wakati timu zinzocheza Shirikisho ni zile zilizomaliza nafasi ya tatu katika ligi zao au kutwaa taji la FA

Mabadiliko hayo yalilenga kuweka uwiano sawa wa ushindani kwenye ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho

Kanuni mpya ilianza kutumika msimu huu ndio maana katika timu zilizoshiriki kombe la Shirikisho kuanzia hatua ya makundi hakuna timu bingwa au iliyomaliza angalau nafasi ya pili kwenye zile nchi ambazo zinatoa timu nne

Pengine mabadiliko haya yamezipa timu unafuu na kufanya vizuri zaidi,  unaweza kusema hili ndio kusudio kuu la mabadiliko ya kanuni hiyo

Hii imeongeza ushindano miongoni mwa timu zinazoshiriki Shirikisho kwani karibu zote zinakuwa katika daraja linalofanana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’