Tumekubali kushindwa msimu huu, tunajipanga kwa msimu ujao - Mkwasa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
11 May 2018
Tumekubali kushindwa msimu huu, tunajipanga kwa msimu ujao - Mkwasa
Baada ya jana Yanga kuuvua rasmi ubingwa uliotwaliwa na wapinzani wao Simba, Katibu wake Mkuu Charles Mkwasa amesema wamekubali kushindwa msimu huu na sasa wanajipanga kwa ajili ya msimu ujao.

Mkwasa amesema kama viongozi wametambua makosa waliyofanya ambayo yamepelekea kufanya vibaya msimu huu na watahakikisha hayajirudii msimu ujao.

"Siwezi kuwasemea wala kuwaambia chochote Simba kwa sababu siku zote adui yako mwombee njaa. Siwezi kusema lolote kwa sababu wenzetu wameanza vizuri, pesa wamezitumia vizuri sisi tumetereza tunakubali yaishe," Mkwasa aliuambia mtandao wa ShaffihDauda.

"Haya ni mashindano ya mwaka mmoja mwaka mwingine yanaanza tena lakini naamini makosa yaliyofanyika Yanga mwaka huu hayawezi kujirudia tena mwaka ujao. Tunaamini mwakani tukiwa na afya njema tutarudi kwenye nafasi yetu."

"Kuna msemo wa Kiswahili unasema ‘kufanya kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa’ kwa hiyo tunakubali kuna makosa ambayo yamefanyika, tumekuwa na wachezaji wenye majeruhi ya muda mrefu tangu tumeanza ligi hatukuwa na mwanzo mzuri tumekuwa tukipata ushindi finyu lakini ndio mwendo wa safari.

"Tunakubali matokeo, tunajipanga kwa ajili ya mwakani"

Yanga iko nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 48 na michezo mitano mkononi.

Baada ya kipigo cha mabao 2-0 kutoka Prisons jana, Yanga iliutema rasmi ubingwa ilioushikilia kwa misimu mitatu mfululizo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →