Mshambuliaji wa Al Nassr Fc ya Saudi Arabia Clara Luvanga amemtembelea na kumpa zawadi ya jezi Rais wa Yanga Injinia Hersi Said
Clara ambaye pia ni mchezaji tegemeo katika timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars), amemtaja Hersi kama miongoni mwa watu waliochangia kumfikisha hapo alipo
Clara aliitumikia Yanga Princess kabla ya kupata nafasi ya kwenda kucheza Arabuni huku uongozi wa Yanga ukimruhusu kuondoka pasipo kulipa gharama yoyote ya ziada

"Ulikuwa ni wakati mzuri nilipokutana na raisi wa club kubwa tanzania Young Africans na Raisi wa vilabu barani africa Hersi Said. Ukweli ninapaswa kujivunia wewe pale ulipo amua kuniachia kwenye timu yako bila kulipa chochote na kwenda kuanza maisha mengine nje ya mipaka ya tanzania shuklani sana," aliandika ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Al Nassr Fc ndio mabingwa wa ligi kuu ya Wanawake Saudi Arabia huku Clara akiwa mfungaji bora wa timu hiyo akifunga mabao 19