Karia akiri sakata la Kariakoo Deby bado halijamalizika

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 May 2025
Karia akiri sakata la Kariakoo Deby bado halijamalizika

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema ripoti kuhusu uchunguzi wa kukwama kwa mchezo wa ligi kuu namba 184 kati ya Yanga dhidi ya Simba uliopaswa kupigwa March 08, itatolewa pale shauri hilo litakapokuwa limekamilika

Jana Karia, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said walikuwa miongoni mwa wageni waalikwa Bunge jijini Dodoma kushuhudia uwasilishaji wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2025 / 2026

Mjadala mkali uliibuka Bungeni ambapo baadhi ya wabunge walihoji uamuzi wa Bodi ya ligi (TPLB) kupangia tarehe mchezo huo kabla ya kutolewa ripoti ya uchunguzi juu ya sababu zilizopelekea mchezo wa kwanza uliopaswa kupigwa March 08 kutofanyika

"Bungeni waliniuliza sana kuhusu ripoti ya uchunguzi, nikawaambia haiwezi kutoka kwasababu kuna mwingine alienda kwenye vyombo vya sheria"

"Kwa sababu kila mmoja ana sehemu yake itafanyika muda utakapofika, shauri bado linaendelea na hatujui litaisha ama halitoisha"

"Kwa hiyo sio vizuri kutoa taarifa hizo kwakuwa tayari mmoja ashaenda sehemu za usuluhisho kwahiyo ni vizuri tukaheshimu," alisema Karia katika mahojiano na Bongo FM

Yanga imetangaza msimamo wake wa kutocheza mchezo huo uliopangwa kupigwa Juni 15 huku pia ikiendelea na harakati za kusaka haki kupitia njia nyingine

Taarifa za ndani zimebainisha kuwa Yanga iliwasilisha malalamiko yake kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ambalo kimsingi ndio wasimamizi wa vyombo vyote vinavyohusiana na masuala ya michezo Tanzania

Baada ya CAS kuitaka Yanga kufungua shauri lake katika mamlaka za soka za ndani kabla ya kuliwasilisha katika mahakama hiyo ya juu zaidi, uongozi wa Yanga umeeleza kutokuwa na imani na TFF ambayo kimsingi ndio wasimamizi wa bodi ya ligi hivyo kuchagua kupeleka malalamiko yao BMT

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’