Wachezaji Yanga wafunguka sababu ya kipigo Mbeya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 May 2018
Wachezaji Yanga wafunguka sababu ya kipigo Mbeya
Baada ya juzi kushuhudia wakiutema rasmi ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara kwa kupokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Tanzania Prisons, baadhi ya wachezaji wa Yanga wamesema ratiba ngumu ya ligi hiyo ndio chanzo cha kufanya vibaya.

Yanga juzi ikiwa ugenini ilikubali kipigo hicho kutoka kwa Tanzania Prisons na kuiacha Simba ikitangaza ubingwa kabla ya kucheza mchezo wake wa leo dhidi ya Singida United.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, beki wa pembeni wa Yanga ambaye alikuwa nahodha kwenye mchezo dhidi ya Prisons, Juma Abdul, alisema kuwa ratiba iliwabana zaidi na kuepelekea wachezaji wengi kuwa na uchovu.

Alisema hawakuwa na muda wa kupumzika pindi wanapotoka kwenye michezo yao ya kimataifa.

"Hata mchezo wa leo (juzi) tumecheza tukiwa na uchovu kwa sababu tulipotoka Algeria tuliunganisha kuja Mbeya, ratiba imechangia sisi kufanya vibaya kwenye michezo yetu ," alisema.

Kauli hiyo pia iliungwa mkono na mshambuliaji wa timu hiyo, Emmanuel Martin, ambaye alisema uchovu umewapa nafasi Tanzania Prisons kuibuka na ushindi.

Matokeo hayo ya juzi yameifanya Yanga kusalia kwenye nafasi ya tatu ikiwa na pointi 48, pointi nne pungufu ya Azam FC wanaoshika nafasi ya pili huku mabingwa wapya, Simba wakiwa na pointi 65.

Nipashe
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
15h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’