Hamdi amepania ushindi dhidi ya Namungo Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 May 2025
Hamdi amepania ushindi dhidi ya Namungo Fc

Baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Jumanne, May 13 katika uwanja wa KMC Complex, Yanga itasubiri zaidi ya mwezi mmoja kuhitimisha mechi zake mbili zitakazokuwa zimebaki kwenye ligi

Mechi mbili za mwisho ni dhidi ya Tanzania Prisons (Mbeya) Juni 18) na dhidi ya Dodoma Jiji (Dar) Juni 22

Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema mechi dhidi ya Namungo Fc siku ya Jumanne ni kama fainali kwani wanahitaji kushinda ili kuwa katika nafasi nzuri na kumaliza vyema mechi hizo mwezi ujao

"Tunakwenda kucheza mechi muhimu dhidi ya Namungo Fc siku ya Jumanne. Hatuna nafasi ya kufanya makosa kwani wapinzani wetu katika mbio za ubingwa wanasubiri tukosee ili wanufaike"

"Tunajua haitakuwa mechi rahisi lakini wachezaji wangu wanafahamu tunahitaji kushinda mchezo huu," alisema Hamdi

Habari njema kwa Yanga kuelekea mchezo huo ni kurejea kikosini kwa wachezaji Khalid Aucho na Pacome Zouzoua ambao walikosa mechi kadhaa za nyuma wakiwa majeruhi

Yanga pia inaweza kupata huduma ya wachezaji kama Prince Dube, Duke Abuya na Clatous Chama ambao walikosekana katika kikosi kilichotwaa taji la Muungano mapema mwezi huu

Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikikusanya alama 70 huku wapinzani wao Simba wakiwa nafasi ya pili na alama 69

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
13h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’