Katika orodha ya vinara 10 wa ufungaji katika ligi kuu ya NBC, ni jina la Clement Mzize pekee kutoka Tanzania aliyefanikiwa kuingia katika orodha hiyo iliyotawaliwa na nyota wa kigeni
Mzize anashika nafasi ya pili katika mbio za ufungaji bora akifunga mabao 13, mabao mawili nyuma ya Jean Ahoua raia wa Ivory Coast anayeitumikia Simba akiwa na mabao 15
Prince Dube (Yanga) na Lionel Ateba (Simba) wanafuata wakiwa na mabao 12 huku Jonathan Sowah (Singida BS), Steven Mukwala (Simba) wakifuatia katika orodha hiyo wakiwa na mabao 11 huku Elvis Rupia (Singida) akifunga mabao 10
Pacome Zouzoua (9), Stephane Aziz Ki (8) na Gibril Sillah wa Azam Fc pia wamo katika orodha hiyo
Unaweza kusema huu ndio msimu bora zaidi kwa Mzize tangu alipopandishwa kikosi cha kwanza kutoka Yanga B misimu mitatu iliyopita
Mzize anayo nafasi ya kuibuka mfungaji bora kama atafunga mabao katika mechi tatu zilizobaki
Faida aliyonayo ni kuwa hana bao alilofunga kupitia mikwaju ya penati tofauti ya Ahoua anayeongoza lakini akiwa na mabao 7 ya penati