Kanuni na taratibu za mpira ziheshimiwe - Mayay

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 May 2025
Kanuni na taratibu za mpira ziheshimiwe - Mayay

Gwiji wa zamani wa Yanga, Taifa Stars na mchambuzi wa soka nchini, Ally Mayay Tembele, amesema alitarajia sakata la kuahirishwa kwa Dabi ya Kariakoo iliyopangwa kuchezwa Machi 8, 2025, lingetatuliwa mapema kutokana na majukumu ya kimataifa yanayolikabili taifa

Mayay amebainisha kuwa Tanzania ni mwenyeji wa michuano ya CHAN 2025, hivyo ni muhimu suala la dabi kumalizwa haraka ili kutoa nafasi ya maandalizi ya kitaifa kufanyika kwa ufanisi

Amependekeza kuwa suluhu ya kudumu ni kuzingatia na kusimamia kanuni, sheria na taratibu zilizowekwa, ili kulinda hadhi ya Ligi Kuu Tanzania Bara

Ikumbukwe kuwa Machi 7 mwaka huu, Simba ilizuiwa kufanya mazoezi ya mwisho na mabausa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, hali iliyosababisha wagome kushiriki mechi

Yanga nayo ikajibu mapigo ya kutocheza tena hadi ilipeleka kesi CAS ikarejeshwa katika mamlaka za soka nchini. Kutokana na uamuzi wa CAS, Bodi ya Ligi imepanga mechi hiyo ichezwe Juni 15, 2025, lakini Yanga imeendelea kusisitiza haitashiriki, jambo linaloibua mashaka na kuathiri taswira ya ligi

Mayay amesema mjadala huo umepamba moto hadi kwenye makundi ya mitandao ya kijamii, jambo linalodhihirisha jinsi gani sakata hilo limegusa hisia za watu wengi Duniani

β€œUbora wa Ligi Kuu ya Tanzania unaweza kuwavutia wawekezaji wa kimataifa, lakini hali kama hii inaweza kuwatisha na kuwafanya waogope kupoteza fedha zao"

"Ni muhimu suala hili litafutiwe suluhu ya haraka kwa mustakabali wa soka letu," alisema Mayay

Aidha, ameongeza kuwa katika enzi zao za uchezaji, hakuwahi kushuhudia mgogoro wa dabi kuwa mkubwa kama ilivyo sasa

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’