Viungo wa Yanga Pacome Zouzoua na Khalid Aucho ni miongoni mwa wachezaji waliojumuishwa katika kikosi kilichosafiri mkoani Tanga kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali kombe la CRDB dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa Jumapili, May 18 katika uwanja wa Mkwakwani
Licha ya kupona changamoto za majeraha, mkufunzi wa Yanga Miloud Hamdi hakuwatumia wachezaji hao katika mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0

Meneja wa Yanga Walter Harrison amethibitisha nyota hao wako fit na tayari kutumika katika mchezo siku ya Jumapili
Aucho na Pacome ni wachezaji muhimu katika kikosi cha kocha Hamdi ambaye mara kadhaa alikiri kuna namna analazimika kubadili mbinu pale anapowakosa wachezaji hao
Hata hivyo upana wa kikosi umeendelea kuinufaisha Yanga kwani chini ya Hamdi, katika mechi 14 wameshinda mechi 13 na kutoka sare mchezo mmoja tu
Hamdi amekuwa huru kufanya 'rotation' ya kikosi chake pasipo kuathiri ubora wa timu