FT : Yanga 2-0 JKT Tanzania, CRDB Cup

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 May 2025
FT : Yanga 2-0 JKT Tanzania, CRDB Cup

Klabu ya Yanga SC imeendelea kuthibitisha ubabe wake katika soka la Tanzania baada ya kuichapa JKT Tanzania mabao 2-0 katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la CRDB, uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Mchezo huo uliokuwa mgumu kutokana na hali ya uwanja kujaa maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha mapema, haukuwa kikwazo kwa Wananchi kuonyesha makali yao na kufuzu kwa fainali ya tano mfululizo ya michuano hiyo maarufu.

Dube na Mudathir Wafungua Mlango wa Fainali

Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na straika wake mahiri Prince Dube, ambaye kwa mara nyingine ameonyesha umuhimu wake katika mechi kubwa. Bao la pili lilifungwa na Mudathir Yahya katika dakika za lala salama, akihakikisha kuwa tiketi ya fainali haibaki ndotoni.

Nafasi Zilizomwagika Kama Maji ya Mvua

Ingawa mabao yalikuwa mawili tu, mchezo huo ulikuwa na nafasi nyingi za wazi ambazo wachezaji wa Yanga kama Stephane Aziz Ki na Maxi Nzengeli walishindwa kuzitumia ipasavyo. Kwa kiwango walichoonyesha, kila mmoja wao alistahili kutoka uwanjani na mpira wa mechi – lakini walikosa bahati.

Sasa Ni Fainali – Muda wa Kujibu Maswali

Kwa matokeo haya, Yanga sasa inasubiri kucheza finali ya Kombe la CRDB. Na kama ujumbe wa mashabiki wa Yanga ulivyo, "bwana yule aliyekimbia Machi 08" sasa hana pa kujificha – kama kweli anataka kucheza na Yanga, fainali ndiyo jukwaa sahihi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’