Aziz Ki ameacha alama Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 May 2025
Aziz Ki ameacha alama Yanga

Kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki ndio hvyo tena, ameondoka Yanga baada ya misimu mitatu ya mafanikio makubwa. Uhamisho wake kwenda Wydad Athletic ya Morocco si tu kwamba umeingizia Yanga takriban TSh bilioni 2, bali pia unampa fursa ya kihistoria ya kucheza Kombe la Dunia la Klabu litakalofanyika mwezi ujao nchini Marekani.

Aziz Ki ameondoka Yanga akiwa na kumbukumbu nzito za mafanikio ya ndani na nje ya uwanja. Akiwasili kama mchezaji huru kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast, aliibuka kuwa mmoja wa wachezaji muhimu waliobadilisha sura ya klabu hiyo na kuipa heshima mpya kisoka, hasa kwenye michuano ya kimataifa.

1. Mchango Wake Kwenye Mabao

Katika michezo 114 aliyocheza katika mashindano yote akiwa na Yanga, Aziz Ki alihusika moja kwa moja kwenye mabao 86. Aliifungia timu mabao 54 na kutoa pasi za mwisho (asisti) 32. Msimu uliopita pekee, alifunga mabao 21 kwenye Ligi Kuu, na hivyo kuwa mfungaji bora wa ligi hiyo, akimzidi Feisal Salum β€˜Fei Toto’ aliyemaliza na mabao 19.

2. Msimu Wake wa Mwisho Ulivyong’ara

Hadi anaondoka msimu huu, Aziz Ki alikuwa tayari amefunga mabao 9 na kutoa asisti 7 kwenye Ligi Kuu. Katika Kombe la FA, alifunga mabao 4, yakiwemo matatu dhidi ya Stand United (hat trick). Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, alifunga mabao manne, mawili kati yake akiwa kwenye hatua ya makundi.

3. Mtaalamu wa Hat Trick

Katika muda wake mfupi nchini, Aziz Ki aliweka rekodi ya kipekee ya kupiga hat trick tano β€” nne kati ya hizo kwenye Ligi Kuu na moja kwenye Kombe la FA. Alianza dhidi ya Kagera Sugar, kisha akazifunga Azam FC na Tanzania Prisons msimu uliopita, na msimu huu akawachapa KMC mabao matatu kabla ya kuwatungua Stand United kwenye FA.

4. Shujaa wa Ushindi wa Kihistoria

Goli lake dhidi ya Club Africain huko Tunisia kwenye Kombe la Shirikisho lilisaidia kuipeleka Yanga hatua ya makundi β€” mafanikio yaliyoipeleka timu hadi fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza. Pia, alifunga goli la utata dhidi ya Mamelodi Sundowns kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa β€” bao ambalo lingeweza kuibeba Yanga hadi nusu fainali kama lingekubaliwa.

5. Mchango wake kwenye Kariakoo Derby

Aziz Ki ameacha kumbukumbu chungu kwa wapinzani wa jadi wa Yanga β€” Simba SC na Azam FC. Aliwafunga Simba mabao matatu, likiwemo goli la freekick kwenye sare ya 1-1, na bao jingine kwenye ushindi wa kihistoria wa 5-1 mnamo Novemba 5, 2023. Pia aliwafunga Azam FC kwenye mechi kadhaa, ikiwa ni pamoja na hat-trick dimba la Mkapa, Oktoba 23, 2023.

Kwa ujumla, Aziz Ki ameacha kumbukumbu ya kipeke kwa Wananchi. Amekuwa zaidi ya mchezaji β€” alikuwa nembo ya mafanikio ya kisasa ya Yanga, akitoa burudani, matokeo, na uongozi wa uwanjani. Uhamisho wake ni ushahidi wa thamani yake barani Afrika na nje, na anabeba jina la Yanga katika anga ya kimataifa.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
23h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’