Ligi Kuu ya Wanawake 2024/25 imefikia tamati jana ambapo Yanga Princess imeshindwa kutamba uwanja wa KMC Complex ikilazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Ceasiaa Queens
Katika msimu ambao Yanga Princess ilianza kwa kusuasua, imemaliza ikiwa nafasi ya tatu baada ya kukusanya alama 39
JKT Queens wameibuka mabingwa wakiwa na alama 47 wakinufaika na mabao mengi ya kufunga mbele ya Simba Queens ambayo pia ilivuna alama 47
Yanga Princess imekuwa katika kipindi cha maboresho bila shaka msimu ujao itarejea ikiwa bora zaidi
Leo Jumatano, tuzo kwa wale waliofanya vyema msimu huu katika kikosi cha Yanga Princess zitatolewa

ADVERTISE HERE