Yanga ulinzi imara, msingi wa mafanikio 2024/2025

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 May 2025
Yanga ulinzi imara, msingi wa mafanikio 2024/2025

Katika msimu wa 2024/2025, Klabu ya Yanga SC imeonesha kwa mara nyingine kuwa si tu timu ya kushambulia, bali pia ina safu ya ulinzi thabiti iliyochangia mafanikio ya Wananchi mpaka sasa.

Kwa mujibu wa takwimu, Yanga imecheza mechi 27 na kuruhusu mabao 10 pekee — hali inayoifanya kuwa timu kinara yenye ulinzi bora zaidi katika ligi kuu ya Tanzania Bara msimu huu

Kuruhusu mabao 10 katika mechi 27 ni sawa na wastani wa bao moja kila baada ya mechi 2.7 — kiwango cha juu cha kiulinzi kinachoashiria umakini mkubwa wa safu ya ulinzi na benchi la ufundi.

Hili ni punguzo kubwa ikilinganishwa na msimu uliopita (2023/2024), ambapo Yanga iliruhusu mabao 14 katika mechi 30, licha ya kuwa na msimu mzuri pia.

Takwimu hizi hazijaja kwa bahati mbaya. Ni zao la nidhamu ya mchezo, maelewano bora baina ya walinzi, na mfumo wa kiufundi unaoifanya Yanga kucheza kwa ushirikiano katika kushambulia na kujilinda

Kwa upande wa ushambuliaji, Yanga haikubaki nyuma pia — ikifunga mabao 71 hadi sasa na kujikusanyia pointi 73, ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi. Hii ina maana moja: uwiano mzuri kati ya kushambulia na kujilinda

Kwa mazingira ya soka la Afrika, ambapo mara nyingi matokeo huamuliwa na makosa madogo ya ulinzi, kuwa na safu ya walinzi imara ni kama kuwa na nusu ya kikombe cha ubingwa mkononi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’