Sillah aitamani Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 May 2025
Sillah aitamani Yanga

Winga wa Azam FC Gibril Sillah katika mahojiano yake ya awali aliwahi kueleza wazi kuwa anatamani siku moja kucheza pamoja na nyota wa Yanga kama Pacome Zouzoua, Stephane Aziz Ki (ambaye sasa yuko Wydad), na Prince Dube aliyewahi kuwa mchezaji mwenzake Azam FC.

Inadaiwa kuwa mkataba wa Sillah na Azam FC unakaribia kufikia mwisho msimu huu, na hadi sasa hajatia saini mkataba mpya na klabu hiyo ya Chamazi.

Mpaka sasa, Yanga bado haijaonyesha nia ya kumsajili winga huyo licha ya kwamba Sillah amewafunga Wananchi mara tatu kwenye mechi mbalimbali za ligi, akithibitisha uwezo wake uwanjani.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe, amesema kwa fahari kuwa kwa sasa kila mchezaji hapa nchini anatamani kuichezea Yanga.

"Sio huyo tu, wachezaji wengi wameomba kusajiliwa Yanga. Tukiamua kuweka majina yao hadharani, kila mtu atashangaa," alisema Kamwe.

"Ni kwa sababu kwa sasa Yanga ndiyo klabu kubwa Tanzania. Tunalipa mishahara mizuri, bonasi, na malipo yote hufanyika kwa wakati."

"Pongezi za kipekee anastahili Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said, kwa kutengeneza mazingira haya, kila mmoja anakumbuka tulivyoteseka miaka ya nyuma" aliongeza Kamwe kwa kujiamini.

Kamwe pia alidokeza kuwa Yanga ina mpango wa kuitembelea Azam FC mara tu dirisha la usajili litakapofunguliwa!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’