Yanga, Msuva kusaka vipaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 May 2025
Yanga, Msuva kusaka vipaji

Katika harakati za kuendeleza na kukuza soka la vijana nchini, klabu ya Yanga SC kwa kushirikiana na Safari Lager, wamemtangaza rasmi mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Saimon Msuva, kuwa Chief Scout wa mashindano ya Safari Lager Cup.

Msuva ataungana na maafisa kutoka Yanga pamoja na Safari Lager kuzindua rasmi shughuli za kusaka vipaji tarehe 30 Mei 2025, jijini Mwanza, ambapo.

Mashindano ya Safari Lager Cup yalizinduliwa rasmi mnamo 7 Mei 2025, yakilenga kuwapa vijana jukwaa la kuonesha uwezo wao wa kisoka. Yanga SC, kama mshirika rasmi wa mashindano haya, imejikita kuunga mkono juhudi hizi kupitia ushirikiano wa karibu na Safari Lager.

Kupitia jukumu lake jipya, Saimon Msuva ataongoza timu ya wataalamu waliobobea katika ufuatiliaji wa vipaji. Watazuru mikoa mbalimbali nchini, wakifanya tathmini ya wachezaji chipukizi, kwa lengo la kuunda kikosi maalum cha Safari Lager ambacho kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Yanga SC mwishoni mwa zoezi hilo la kusaka vipaji.

Saimon Msuva ni jina linaloheshimika sana ndani ya historia ya Yanga SC. Alitoa mchango mkubwa katika mafanikio ya klabu hiyo kabla ya kwenda nje ya nchi kutafuta mafanikio zaidi kisoka

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’