Singida BS yatishia kugomea mechi dhidi ya Simba, kujitoa ligi kuu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 May 2025
Singida BS yatishia kugomea mechi dhidi ya Simba, kujitoa ligi kuu

Klabu ya Singida BS imetishia haitacheza mechi ya nusu fainali ya kombe la CRDB dhidi y Simba iliyopangwa kupigwa Jumamosi May 31 endapo mchezo huo utachezeshwa na waamuzi wenye mashaka nao

Aidha klabu hiyo imeitaka Bodi ya Ligi/TFF kumchukulia hatua mwamuzi Elly Sasie kufuatia matukio ya kutoitendea haki timu hiyo katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa juzi Jumatano katika uwanja wa KMC Complex

Katika mchezo huo ambao Singida BS ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0, kuna matukio matatu ambayo Sasie 'alimeza filimbi' akiwanyima walima alizeti hao mikwaju ya penati

Akizungumza na chombo kimoja cha habari jana, msemaji wa Singida Black Stars, Hussein Massanza alisema wameiandikia barua Bodi ya ligi na wanataka kujibiwa kinyume na hivyo watajitoa kushiriki ligi kuu na michuano ya kombe la CRDB

"Baada ya kujiridhisha kuna matukio hayakuamuliwa kwa haki kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba Sc jana,tumewasilisha barua ya malalamiko kwa mamlaka husika kwa mujibu wa kanuni na kueleza msimamo wetu kama klabu"

"Tunataka mamlaka zimchukulie hatua mwamuzi Elly Sasie kwa kile alichotufanyia katika mchezo huo. Lakini pia tumeitaka mamlaka isitupangie waamuzi ambao tuna mashaka nao kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la CRDB dhidi ya Simba"

"Kama mamlaka hazitafanyia kazi malalamiko yetu basi tutajiondoa kushiriki ligi kuu ya NBC pamoja na kombe la CRDB. Tutatafuta kwingine ambako tutashiriki ligi inayoendeshwa kwa haki hata kama ni Zanzibar," alisema Massanza

Malalamiko hayo ya Singida BS yanajitokeza huku kukiwa na taarifa baadhi ya timu zimetishia kutocheza mechi mbili zilizosalia kuhitimisha msimu huu baada ya kutoridhishwa na mwenendo mzima wa uendeshaji wa ligi

Mpaka sasa timu zilizofikia uamuzi huo wa kususia ligi zimefika 6

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’