Edna Lema atamani kufundisha timu ya Wanaume

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 May 2025
Edna Lema atamani kufundisha timu ya Wanaume

Kocha wa Yanga Princess, Edna Lema, ametangaza wazi kuwa anaweza akastaafu kazi ya ukocha ndani ya miaka mitano ijayo endapo hatopata nafasi ya kufundisha timu ya wanaume katika Ligi Kuu au Championship.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii, Edna amesema kuwa malengo yake makubwa ya sasa ni kupanda ngazi katika taaluma ya ukocha na kupata changamoto mpya nje ya Tanzania, huku akisisitiza kuwa ana kiu ya kujifunza zaidi kupitia vitendo na si nadharia pekee.

"Kama ndani ya hii miaka mitano Mungu akinijalia afya njema, kama sitakuwa nimefundisha timu yoyote ya wanaume ya Championship au Ligi Kuu kama kocha mkuu, basi nitaachana kabisa na kufundisha mpira. Nitafanya kazi nyingine za mpira, lakini si ukocha," amesema.

Edna pia ameweka wazi kuwa iwapo hatopata nafasi hiyo hapa nchini, basi yuko tayari kwenda kutafuta changamoto mpya nje ya mipaka ya Tanzania.

"Sina kitu kingine cha kujifunza nikiwa hapa tena. Natakiwa kwenda kufundisha nje ili nijue ugumu wake na urahisi wake. Nikiwa najifunza kukosea ndio kupatia,” aliongeza Edna, akionesha dhamira yake ya kweli ya kutafuta mafanikio zaidi katika kazi ya ukocha.

Kwa muda mrefu, Edna Lema amekuwa miongoni mwa makocha wanawake wachache wanaopambana kupenya katika medani ya mpira wa miguu wa wanaume, jambo ambalo bado ni nadra barani Afrika.

Edna amekamilisha mafunzo ya kupata leseni A ya CAF ambayo itamuwezesha kufundisha timu ya ligi kuu ndani na hata nje ya Tanzania

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’