Simu zitaendelea kuita sana..

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jun 2025
Simu zitaendelea kuita sana..

Katika kile kinachoonekana kuwa mwendelezo wa kuimarisha kikosi kuelekea msimu ujao, Klabu ya Yanga SC inatajwa kumuongezea mkataba mpya kiungo wao mahiri, Mudathir Yahya.

Nyota huyo kutoka Zanzibar ameongeza mkataba wa miaka miwil, hatua inayowapa Wananchi matumaini ya kuendelea kuona ubora wake katika viunga vya Jangwani.

Mudathir ni mmoja wa wachezaji wanaomaliza mikataba mwishoni mwa msimu huu, mabosi wa Yanga tayari wamemalizana nae na kilichosalia ni tangazo rasmi kutoka kwa klabu.

Uamuzi huo umechochewa na kiwango bora anachoendelea kukionyesha msimu huu licha ya changamoto za kiufundi na mabadiliko ya majukumu ndani ya kikosi.

Akiwa na umri wa miaka 29, Mudathir amekuwa mhimili wa kati wa kikosi cha Yanga katika misimu mitatu iliyopita, kipindi ambacho klabu hiyo imekuwa ikitawala soka la Tanzania.

Msimu uliopita ulikuwa wa mafanikio binafsi kwake, alipofanikiwa kupachika mabao 9 katika Ligi Kuu ya NBC, rekodi bora kwake kama kiungo wa kati.

Hata hivyo, msimu huu idadi ya mabao imepungua, akiwa ameweza kufunga mabao 2 pekee hadi sasa. Lakini hiyo haimaanishi kuporomoka kwa kiwango, pengine imechangiwa na kubadilika kimajukumu uwanjani.

Kutokuwepo mara kwa mara kwa Khalid Aucho kutokana na majeraha, kumemlazimu Mudathir kujikita zaidi kwenye jukumu la kiungo mkabaji badala ya kupanda na kushuka kama alivyozoeleka

Kwa nyakati tofauti, Mudathir amecheza sambamba na Duke Abuya ambaye naye amekuwa na msimu wa kipekee. Hii imemfanya Mudathir kuwa mchezaji anayechukua majukumu tofauti kwa mujibu wa mahitaji ya timu

Mudathir amewahakikishia mashabiki wa Yanga kuwa ataendelea kujituma na kuipigania timu hiyo kwa nguvu zote. Amedokeza kuwa “simu zitaendelea kuita kama kawaida”

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’