Yule kiungo aliyekuwa anakaribia kujiunga na klabu ya Simba, Pius Buswita kutoka Mbao FC amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga.
Yanga ndio iliyokuwa ya kwanza kufanya mazungumzo na mchezaji huyo lakini ukata wa fedha ukapelekea mahasimu wao Simba wakateka mchakato na kufanya nae mazungumzo yaliyokuwa kwenye hatua za mwisho.
Hata hivyo Yanga inayoonekana kuimarika kiuchumi sasa imemsajili mchezaji huyo dakika za mwisho wakati viongozi wa Simba wakihaha kusaka pesa za usajili kulingana na mtandao wa SalehJembe.

“Simba walikubaliana kila kitu, likabaki suala la kusaini tu. Lakini wakawa hawana fedha,†kilieleza chanzo cha mtandao huo.
“Yanga wameitumia nafasi hiyo kuwagaragaza Simba na kumsainisha.â€
Huyo anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Yanga wakati mahasimu wao Simba tayari wamesajili wachezaji nane.

ADVERTISE HERE