Msemaji wa zamani wa Yanga Haji Manara ameachiwa kwa dhamana hii leo Ijumaa baada ya kufika katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central) kufuatia wito wa Jeshi la Polisi kwaajili ya mahojiano.
Manara ambaye kwa sasa ni Mwanachama wa kawaida wa Yanga, alihojiwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumdhalilisha Rais wa TFF, Wallace Karia mtandaoni
Manara aliandika jumbe mbalimbali katika ukurasa wake wa mitandao wa Instagram baada ya Yanga kuibua madai ya kutolipwa fedha za ubingwa wa kombe la CRDB msimu uliopita
Taarifa kutoka Jeshi la Polisi imeeleza uchunguzi bado unaendelea, ambapo Manara alitoa maelezo kwa maandishi
Hii itakuwa mara ya pili kwa Manara kuingia katika mvutano na Rais wa TFF akitokea kutumikia kifungo cha soka cha miaka miwili baada ya yale yaliyotokea kwenye mchezo wa fainali kombe la FA kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union mkoani Arusha mwaka 2022