Kikosi cha Yanga leo asubuhi kilikamilisha maandalizi kabla ya kuanza safari kuelekea mkoani Mbeya tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons
Jumatano, Juni 18 Yanga itashuka wa Sokoine kuikabili Prisons katika mchezo ambao Wananchi wanazihitaji alama zote tatu ili kuendelea kusogelea ubingwa wa 31 ligi kuu ya NBC
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema wameuchukulia mchezo huo kwa umuhimu mkubwa ikizingatiwa wanahitaji kushinda
Amewataka mashabiki wa timu hiyo mkoani Mbeya na maeneo ya jirani kuwa tayari kuipokea timu na kujitokeza kwa wingi uwanja wa Sokoine siku ya Jumatano 'kuhanikiza' msako wa alama tatu muhimu
Ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kukusanya alama 73 katika mechi 27, Yanga inahitaji kushinda mechi mbili zinazofuata kabla ya kuhitimisha msimu dhidi ya watani zao Simba Juni 25
Kama Yanga itakusanya alama 6 kutoka mechi mbili zinazofuata, kwenye mchezo dhidi ya Simba itahitaji angalau sare tu ili kutwaa ubingwa