Walitaka ubingwa bila kumkaba Pacome?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Jun 2025
Walitaka ubingwa bila kumkaba Pacome?

Uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine jana uligeuka uwanja wa mazoezi kwa Yanga SC baada ya Wananchi kuichakaza Tanzania Prisons kwa mabao 5-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Huu si ushindi wa kawaida tu, ulikuwa ni ujumbe mzito uliotumwa moja kwa moja kwenda kwa watani zao Simba SC ambao licha ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya vibonde Ken Gold walioshuka daraja, walikosa furaha

Yanga wameonyesha dhamira yao ya kulitaka Jangwani taji la nne mfululizo ligi kuu ya NBC. Mara nyingi uwanja wa Sokoine umekuwa mgumu kwao, lakini safari hii vijana wa Miloud Hamdi walionekana kana kwamba wako mazoezini tu. Idadi ya mabao ilikuwa tano, lakini wangeweza kufunga hata mara saba au zaidi kama wangetumia nafasi zao vyema.

Nyota wa mchezo, Pacome Zouzoua, alionyesha tena kwamba yeye ni zaidi ya mchezaji wa kawaida, ni hatari ya wazi kwa timu yoyote inayomkabili.

Alifunga mabao mawili, akafikisha jumla ya mabao 11 msimu huu pamoja na pasi 9 za mabao. Mchezaji huyu si tu chachu ya mafanikio ya Yanga, bali ni kitendawili kigumu ambacho Simba italazimika kukitatua ifikapo Juni 25 kwenye Dabi ya Kariakoo.

Mashabiki wa Yanga wanasema wazi: "Kama Simba wanadhani wanaweza kutwaa ubingwa bila kumkaba Pacome, basi wajue tayari wamepotea."

Baada ya kipigo kwa Prisons, Yanga wanarejea Dar kisha kuelekea Zanzibar kumenyana na Dodoma Jiji katika mchezo wa mwisho kabla ya dabi.

Maandalizi ya mwisho yatafanyika Visiwani humo, wakijipanga kwa mtanange wa kumaliza msimu dhidi ya Simba, mchezo ambao utakuwa na maana kubwa zaidi ya pointi tatu:

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’