TPLB yajaza nafasi ya Mnguto, Kasongo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jun 2025
TPLB yajaza nafasi ya Mnguto, Kasongo

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya mabadiliko muhimu katika safu yake ya uongozi kufuatia kuondoka kwa viongozi wawili wakuu, Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu waliotoka kwenye nafasi hizo kwa sababu tofauti mnamo Juni 13, 2025.

Katika hatua ya kuhakikisha utendaji wa bodi haukwami, TPLB imemteua Makamu Mwenyekiti wake, Nassor Idrissa ‘Father’, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Azam FC, kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa bodi hiyo. Nafasi hiyo iliachwa wazi baada ya aliyekuwa Mwenyekiti, Steven Mnguto, kujiuzulu rasmi kwa barua mwishoni mwa juma lililopita.

Kwa upande mwingine, nafasi ya Mtendaji Mkuu wa TPLB imejazwa kwa muda na Ibrahim Mwayela, aliyekuwa Meneja Fedha wa bodi hiyo. Mwayela atakaimu nafasi hiyo kufuatia kusimamishwa kazi kwa Almas Kasongo na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia

Kupitia barua rasmi kwa klabu zote wanachama, TPLB ilieleza:

“Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inakujulisha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Nassor Idrissa amekaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo kwa mujibu wa ibara 33:5 ya Kanuni za Uongozi za TPLB.

“Katika hatua nyingine, Meneja Fedha wa TPLB, CPA Ibrahim Mwayela ameteuliwa kukaimu nafasi ya Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), baada ya Almasi Kasongo kusimamishwa kazi mwishoni mwa juma lililopita. Bodi inatarajia ushirikiano wa dhati wa klabu yako kwa viongozi hao.”

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’