Yanga imeendeleza ubabe ligi kuu ya NBC leo ikiifumua Dodoma Jiji mabao 5-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar
Ni mchezo wa pili mfululizo Yanga inaibuka na ushindi wa mabao 5-0 sasa wakifunga mabao 10 katika mechi mbili tu
Clatous Chama alifungua kalamu ya mabao kabla ya Duke Abuya, Ibrahim Bacca na Maxi Nzengeli kufunga mengine matatu katika kipindi cha pili huku Joash Onyango akijifunga bao jingine
Alama 79 kileleni na sasa umebaki mchezo mmoja tu dhidi ya Simba Juni 25 Yanga ikihitaji angalau alama moja kutetea ubingwa
ADVERTISE HERE