Kama Yanga ilikuwa na mpango wa kuachana na kiungo kiraka Duke Abuya raia wa Kenya basi huenda mpango huo ukawa umefutika jana baada ya kiwango bora alichoonyesha katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Katika mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kutetea taji la ligi kuu kwa msimu wa nne mfululizo, Abuya ambaye kocha Miloud Hamdi alimuanzisha badala ya Clatou Chama kinyume na matarajio ya wengi, 'aliteka shoo' katika eneo la kiungo akishirikiana vyema na Mudathir Yahya, Khalid Aucho na Maxi Nzengeli
Abuya alionekana kila mahali akikaba, kupora mipira na kupiga pasi za uhakika, utulivu wake anapokuwa na mpira mguu ni kitu kilichowafurahisha wengi
Hamdi jana aliifunga Simba kupitia nguvu aliyowekeza katika eneo la kiungo, Abuya ni moja ya silaha zilizomhakikishia anapata kile alichokitaka katika mchezo huo
Yanga inatarajiwa kufanya maboresho katika eneo lake la kiungo ambapo hivi karibuni ilimshusha nchini kiungo fundi namba nane Mohamed Doumbia raia wa Ivory Coast ambaye ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba kunako klabu ya SC Majestic ya Burkina Faso
Abuya amemshawishi kocha Miloud Hamdi na bila shaka atamuhitaji kuendelea nae katika kikosi chake msimu ujao
