Yanga kuwabana wachezaji kwenye mikataba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 May 2018
Yanga kuwabana wachezaji kwenye mikataba
Moja ya mambo yaliyoiathiri Yanga msimu huu ni kusajili wachezaji kwa gharama kubwa halafu wakashindwa kuisaidia timu.

Jambo hili limewagutusha viongozi ambao sasa wameapa kuongeza umakini kwenye usajili wa mwaka huu.

Viongozi hao wamedhamiria kuweka vipengele kwenye mikataba mipya vikavyoweka maslahi sawa kwa pande zote mbili yanapotokea mazingira ya utata kama ilivyotokea kwa baadhi ya wachezaji msimu huu.

Imeelezwa Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amependekeza mikataba ya wachezaji iwe na vipengele vinavyoruhusu mikataba hiyo kupitiwa kila baada ya miezi sita.

Ili kuweza kuwanufaisha zaidi wachezaji wanaofanya vizuri lakini pia kuwabana wachezaji ambao hawafanyi vizuri kulingana na maslahi ya mikataba yao.

Uongozi wa Yanga unasubiri mapendekezo ya Zahera ili kuanza zoezi la kuisuka upya timu hiyo iliyokumbwa na misukosuko mingi msimu huu.

Taarifa zaidi zinabainisha kuwa kocha huyo ameahidi kukabidhi ripoti yake kwa uongozi baada ya mchezo dhidi ya Rayon Sports kesho.

Wadadisi wa mambo wanatabiri

Kwa mwenendo aliouonyesha Zahera katika siku zake chache akiwa na kikosi cha Yanga, huenda akashusha 'panga kali' kwa idadi kubwa ya wachezaji.

Hivi karibuni katika mahojiano yake na gazeti la Mwanaspoti, Zahera alibainisha kuvutiwa na wachezaji wawili miongoni mwa sita wa Kimataifa na pia kushangazwa kuwepo kwa idadi kubwa ya wachezaji ambao 'hawana hadhi' ya kuitumikia timu hiyo.

Kocha huyo alibainisha kuwa ndani ya kikosi cha Yanga wamo wachezaji wazuri ambao wanahitaji kuimarishwa zaidi lakini wapo ambao hawastahili kuwepo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4m ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
14h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
18h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
19h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
19h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’