Sowah awapa hofu mashabiki Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Jul 2025
Sowah awapa hofu mashabiki Yanga

Siku chache tu baada ya mchezo wa fainali ya Kombe la CRDB kati ya Singida Black Stars na Yanga SC, jina la mshambuliaji Jonathan Sowah limeendelea kuvuma mitandaoni lakini si kwa sababu nzuri.

Tukio la mchezaji huyo wa Singida kutolewa nje kwa kadi nyekundu limezua maswali mengi, hasa kwa mashabiki wa Yanga ambao timu yao inahusishwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo raia wa Ghana.

Katika dakika za lala salama za mchezo huo uliopigwa visiwani Zanzibar, Sowah alionyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje na mwamuzi Ahmed Arajiga, baada ya kutupa mpira kwa hasira kufuatia kunyimwa mpira wa kona.

Hii ilikuwa baada ya awali kupewa kadi ya kwanza ya njano kwa kumchezea madhambi beki wa Yanga, Ibrahim Bacca, ambaye alimkaba vilivyo na kumzuia kung’ara uwanjani.

Tukio hilo limewakumbusha mashabiki wa Yanga tukio lingine la aina hiyo msimu mmoja uliopita wakati Sowah akiitumikia Medeama SC ya Ghana. Katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga uliopigwa jijini Dar es Salaam, Sowah alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa tukio linalofanana.

Mitandaoni, baadhi ya mashabiki wa Yanga wameanza kueleza mashaka yao kuhusu nidhamu ya mchezaji huyo. Ujumbe mmoja kwenye mtandao ulisema:

"Sowah ni mshambuliaji mzuri lakini nina mashaka na nidhamu yake, kama Yanga inamsajili inafaa ashauriwe kupunguza hasira, bila hivyo ni mchezaji ambaye anaweza kuigharimu timu wakati wowote."

Sowah, ambaye kwa sasa anahusishwa kwa karibu na uhamisho kuelekea Yanga SC kuchukua nafasi ya Kennedy Musonda aliyemaliza mkataba, anaonekana kuwa na changamoto katika kudhibiti hisia zake, hasa katika mechi za presha kubwa.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’