Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amewashukuru Wananchi kwa ushiriano aliopata katika kipindi kifupi alichoitumikia Yanga
Juzi klabu ya Ismailia ya Misri ilimtambulisha Hamdi ambaye alimaliza msimu na Yanga kibabe akitwaa mataji matatu
Kupitia ujumbe alioandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Hamdi amesema halikuwa jambo rahisi kwake kufikia uamuzi huo wa kuondoka lakini anaheshimu uamuzi wa klabu
"Ndugu Wananchi nilitaka kuwashukuru sana kwa sapoti yenu, uwepo wenu wa kudumu pembeni yetu. Nilitaka kuwashukuru kutoka ndani ya moyo wangu kwa furaha na shangwe zote mlizotupa"
"Mmenigusa sana na machozi yalinitiririka wakati wa gwaride, mlikuwa wazuri na nikajisemea wakati wa gwaride lakini ni fahari gani kushinda mataji haya kwa ajili yenu"
"Naheshimu uamuzi w klabu, nawtakia kheri nyingi na mafanikio msimu ujao, najua kwa nini nilijiwekeza mwili na roho kwa ajili yenu, mnastahili sana, nawapenda na kamwe sitawasahau, nyie ni bora zaidi," aliandika Hamdi
Hamdi amekuwa kiocha aliyepata mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi alioitumikia Yanga. Lakini pia ameacha takwimu za kutisha akiiongoza Yanga katika mechi 21 kwenye mashindano yote huku akishinda mechi 20