Yanga, Ecua ni suala la muda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Jul 2025
Yanga, Ecua ni suala la muda

Klabu ya Yanga SC inatajwa kukamilisha dili la kiungo mshambuliaji kutoka Zoman FC, Celestin Ecua (23), ambaye msimu uliopita aliitumikia ASEC Mimosas kwa mkopo.

Hatimaye, ndoto ya mashabiki wa Wananchi kuona nyota huyo akivaa jezi ya kijani na njano imekaribia kuwa halisi, akisubiri kutambulishwa rasmi.

Jina la Ecua limetajwa sana kwenye kinyang’anyiro cha usajili, lakini Yanga wameonesha dhamira ya kweli na kufanikisha dili hilo mbele ya vigogo wengine wa soka nchini Tanzania waliokuwa wakimwania.

Katika msimu wake wa mwisho akiwa ASEC Mimosas, Ecua alionyesha kiwango cha juu kwa kufunga mabao 15 na kutoa assists 12 katika michuano yote . Ni takwimu ambazo si tu zinaashiria uwezo wake wa kumalizia, bali pia ubunifu wake katika kutoa pasi za mabao.

Kinachomfanya kuwa lulu zaidi kwa Yanga ni uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi ndani ya uwanja. Ecua ni mchezaji anayetumia zaidi mguu wa kushoto, ana kasi, mbunifu, na mwenye uwezo wa kucheza kama winga wa pande zote au kiungo mshambuliaji namba 10. Aina hii ya mchezaji huwapa makocha nafasi kubwa ya mbinu tofauti kulingana na mechi wanazokutana nazo.

Inaelezwa Ecua huenda atachukua nafasi ya Mcongomani Jonathan Ikangalombo, ambaye licha ya kutua Jangwani dirisha dogo lililopita akitokea AS Vita, hakufanikiwa kuwashawishi mabosi wa Yanga.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’