Mlinzi wa kulia wa Yanga Yao Kouassi raia wa Ivory Coast, ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania, imefahamika
Licha ya kuongeza mkataba, Yao ataendelea kuwa nje kuuguza jeraha la goti baada ya kufanyiwa upasuaji mwezi May nchini Morocco
Taarifa ya awali ya matibabu yake ilibainisha kuwa alipaswa kuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi sita lakini baada ya miezi miwili, Yanga imepata matumani mapya kuwa anaweza kurejea uwanjani mapema
Wiki iliyopita Yao alikuwa nchini kusherehekea shamra shamra za mataji ya Yanga na wachezaji wenzake
Ni wazi sasa Yanga imeachana na mpango wa kusajili beki mwingine wa kulia kwani Israel Mwenda amefanikiwa kuziba pengo la Yao akisaidiana na Kibwana Shomari
ADVERTISE HERE