Tusiogope mabadiliko, tutaumbuka Waungwana

Muungwana wa Yanga By Muungwana wa Yanga
β€’
17 May 2018
Tusiogope mabadiliko, tutaumbuka Waungwana
Yanga inapita katika kipindi kigumu sasa pengine kuliko wakati mwingine wowote.

Sina kumbukumbu za hivi karibuni za Yanga kucheza michezo nane sawa na dakika 720 mfululizo bila ya kupata ushindi, hilo limetokea wakati huu.

Lakini kila jambo linatokea kwa sababu. Huenda mwenendo huu ukawa chachu ya kuyakimbilia mabadiliko makubwa ya kimfumo.

Hakuna namna Yanga itafanikiwa kama haitabadili mfumo wake na kujiendesha.

Jana Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara, alizungumza ukweli ambao viongozi wa vilabu vyetu huwa hawapendi kuusikia.

Kwa muda mrefu vilabu vyetu vimekuwa vikiendeshwa kwa mifumo ya 'kisanii' ambayo haina manufaa makubwa kwa timu. Zaidi ya kunufaisha watu wachache.

Tuache woga, timu zote kubwa duniani zinamilikiwa na matajiri. Sisi wanachama hatuwezi kuziendesha timu, huo ndio ukweli.

Tumejaribu kwa zaidi ya miaka 80 na tumeshindwa na ukweli ni kwamba hatutaweza milele.

Hata wadhamini tulionao hawana uwezo wa kutimiza mahitaji yote ya timu.

Njia pekee ya sisi kuondoka hapa tulipo kwanza tufanye mabadiliko tena haraka kwa kuwa muda hauko upande wetu.

Kuna hatari ya kuingia msimu mpya tukiwa na hali hii hii kama hatutachukua hatua haraka kwa kuwa Yanga inakabiliwa na mashindano mengi kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

Michuano hii ya kombe la Shirikisho itamalizika Agosti 29, wakati ambao tayari msimu mpya utakuwa umeanza.

Kati ya Juni na Julai kuna mashindano ya kombe la Kagame na yale ya Sportpesa ambayo naamini Yanga itashiriki.

Yanga inahitaji kuimarishwa hivyo tujipange mapema ili tuwe na muda wa kufanya marekebisho hayo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’