Marioo, Dogo Pattern kupamba fainali Yanga vs Safari Lager

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jul 2025
Marioo, Dogo Pattern kupamba fainali Yanga vs Safari Lager

Msanii maarufu wa Bongo Fleva, Omari Ally maarufu kama Marioo, pamoja na mkali wa muziki wa Singeli, Dogo Pattern, wanatarajiwa kupamba tamasha la fainali ya Safari Lager Cup litakalofanyika Julai 26 mwaka huu katika uwanja wa KMC Complex.

Mchezo huo wa fainali utawakutanisha mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC, dhidi ya timu ya Safari Lager Talents, ambayo imekusanya vijana chipukizi kutoka sehemu mbalimbali nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Safari Lager, Pamela Kikui, amesema maandalizi kuelekea fainali hiyo yamekamilika kwa asilimia 100 huku akitoa wito kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi kufurahia burudani ya mpira na muziki.

“Ili kunogesha fainali hiyo, tutakuwa na burudani kabambe kutoka kwa Marioo na Dogo Pattern. Tunaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi kushuhudia vipaji vya vijana wetu pamoja na kusheherekea kwa muziki wa wasanii wetu wakubwa,” amesema Kikui.

Kwa upande wake, Meneja wa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe, amesema kabla ya mechi hiyo kutakuwepo na mchezo wa ufunguzi kati ya mashabiki wa Yanga dhidi ya wasanii mbalimbali akiwemo wa muziki, vichekesho, na waigizaji maarufu.

“Mchezo huu wa kirafiki utakuwa sehemu ya burudani ya awali, tunawaomba mashabiki waje kwa wingi kushuhudia burudani hii ya kipekee kabla ya fainali yenyewe,” amesema Kamwe.

Ameongeza kuwa tiketi za mchezo huo tayari zimeanza kuuzwa na amewataka mashabiki kununua mapema ili kuepuka usumbufu siku ya mchezo.

Naye, Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Ibrahim Mohamed, amewataka vijana wa timu ya Safari Lager Talents kuchangamkia mafunzo wanayopata kutoka kwa wachezaji wa zamani kwani hiyo ndiyo njia ya kufanikisha ndoto zao.

“Kwa upande wetu, tupo kwa ajili ya kuinua vipaji. Tukiwaona mna uwezo wa kweli, hatutawaacha; tutawapa nafasi rasmi ili muendelee katika ngazi ya juu zaidi,” amesema Mohamed.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
48m ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
12h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
16h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
21h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’